Survey privacy notice - Swahili

UTANGULIZI

Karibu katika ilani ya faragha ya Utafiti wa Yonder Consulting Limited. Yonder Data Solutions ni jina la biashara la Yonder Consulting Limited.

Yonder inaheshimu faragha yako na imejitolea kulinda data yako binafsi. Ilani hii ya faragha itakuarifu jinsi ya kuangalia data yako ya binafsi wakati unashiriki katika tafiti zetu na kukuambia kuhusu haki zako za faragha na jinsi sheria inavyokulinda.

Ilani hii ya faragha haitumiki kwa ukusanyaji na uchakataji wetu wa data binafsi zinazohusiana na tovuti hii. Kama ungependa kufahamu jinsi Yonder inavykusanya na kuchakata data yako ya binafsi wakati unapotembelea tovuti, tafadhali soma Ilani ya Faragha ya Tovuti yetu.Pia, kama unatupatia data mtandaoni kama mshiriki wa paneli la .Y Live, Ilani yetu ya Faragha ya .Y Live itatumika badala ya ilani ya faragha.

Yonder inatekeleza utafiti wa soko kwa niaba ya wateja wake. Ilani hii ya faragha inatumika kwa utafiti ambapo Yonder ni mdhibiti wa data kulingana ya utafiti husika.

ยท Kama Yonder pekee inaamua ni nani anashiriki katika utafiti na ni maswali gani yanaulizwa basi Yonder itakuwa mdhibiti pekee wa data wa utafiti na ilani hii ya faragha itatumika pamoja na ilani zingine zilizotolewa mwanzoni wa utafiti.

ยทKama Yonder na wateja wake wanashiriki majukumu kwa kuamua ni nani anashiriki kwenye utafiti na ni maswali gani yanaulizwa basi tutakuwa wadhibitiwenza pamoja na mteja mmoja au zaidi na ilani hii ya faragha itatumika pamoja na ilani zingine zilizotolewa mwanzoni wa utafiti, ambazo zinaweza kujumuisha ilani ya faragha ya mteja wetu.

ยท Kama wateja wetu wanabaki udhibiti wa jumla kuhusu ni nani anashiriki katika utafiti na ni maswali gani yanaulizwa na tunatenda pekee kwa maelezo ya mteja wetu, basi Yonder itakuwa mchakataji wa data ya utafiti na siyo mdhibiti wa data na ilani hii ya faragha haitatumika, ni ilani zilizotolewa mwanzoni wa utafiti pekee.

Tutakuambia mwanzoni wa utafiti endapo Yonder inatenda kama mdhibiti wa kipekee, mdhibiti wa ushirikiano au mchakataji wa data wa utafiti husika. Endapo sisi si wadhibiti wa data, au sio mdhibiti pekee wa data, bado tutakuambia wadhibiti wa data ni nani.

Ilani hii ya faragha imetolewa kwa muundo wa tabaka ili uweze kubofya kwenye sehemu mahususi zilizopangwa hapo chini. Tafadhali pia tumia Faharasa kuelewa maana ya baadhi ya maneno yaliyotumiwa katika ilani hii ya faragha.

1. TAARIFA MUHIMU NA SISI NI KINA NANI

2. DATA TUNAZOKUSANYA KUKUHUSU
3. DATA YAKO YBINAFSI INAKUSANYWA KWA JINSIGANI
4. JINSI TUNAVYOTUMIA DATA YAKO BINAFSI
5. UFICHUZI WA DATA YAKO BINAFSI
6. UHAMISHAJI WA KIMATAIFA
7. USALAMA WA DATA
8. UHIFADHI WA DATA
9. HAKI ZAKO ZA KISHERIA
10. FAHARASA

1. TAARIFA MUHIMU NA SISI NI KINA NANI

1.1 Lengo la Ilanihii ya Faragha

Ilani hii ya faragha inalenga kukupatia taarifa kuhusu jinsi Yonder inakusanya na kuchakata data yako binafsi wakati unashiriki katika tafiti zetu.

Ni muhimu kwamba unasoma ilani hii ya faragha pamoja na ilani nyingine ya faragha au ilani ya uchakataji wa haki tunaweza kutoa katika matukio maalum wakati tunakusanya au kuchakata data binafsi kukuhusu ili uweze kutambua kikamilifu kwa jinsi gani na ni kwa nini tunatumia data yako. Ilani hii ya faragha inakamilisha ilani zingine na haijalenga kuzighairi.

1.2 Mdhibiti

Yonder Consulting Limited ni mdhibiti na anawajibikia data yako binafsi (kwa pamoja inatambulika kama โ€œYonderโ€, โ€œsisiโ€, โ€œsisiโ€ au โ€œyetuโ€ katika ilani hii ya faragha).

Tumeteua ofisa wa ulinzi wa data (DPO) ambaye anashughulikia maswala ya maswali yanayohusiana na ilani hii ya faragha. Kama una maswali yeyote kuhusu ilani hii ya faragha, ikiwemo maombi yoyote ya kutumia haki zako za kisheria, tafadhali wasiliana na DPO kwa kutumia maelezo yaliyotolewa hapo chini.

1.3 Maelezo ya Mawasiliano

Jina la kampuni: Yonder Consulting Limited

Jina au cheo cha DPO: Mike Wooderson

Anwani ya Barua pepe: dataprotection@yonderconsulting.com

Anwani ya posta: Northburgh House, 10 Northburgh Street, London, EC1V 0AT

Una haki ya kutoa malalamiko wakati wowote kwenye Ofisi ya Kamishna wa Taarifa (ICO), mamlaka ya Uingereza ya usimamizi wa maswala ya ulinzi wa data (www.ico.org.uk). Hata hivyo, tutashukuru kupata fursa ya kushughulikia maswali yako kabla ya kufikia ICO, basi tafadhali wasiliana nasi kwanza.

1.4 Mabadiliko kwa Notisi ya Faragha na Jukumu lako kutuarifu kuhusu Mabadiliko

Toleo hili lilisasishwa mnamo Mei 2018 na linaweza kupatikana kwa kuwasiliana nasi.

Ni muhimu kwamba data binafsi tuliyonayo kukuhusu ni sahihi na imesasishwa. Tafadhali tujulishe kama data yako binafsi inabadilika wakati wa uhusiano wako nasi.

1.5 Viungo vya Wahusika Wengine

Tovuti hii inaweza kujumuisha viungo kwenda kwenye tovuti za wahusika wengine, vipandiko na programu. Kubofya kwenye viungo hivyo au kuwezesha viungo hivyo kunaweza kuwezesha wahusika wengine kukusanya na kushiriki data kukuhusu. Hatudhibiti tovuti hizi za wahusika wengine na hatuwajibiki kwa maelezo yao ya faragha. Unapoondoka kwenye tovuti yetu, tunakuhimiza kusoma ilani ya faragha ya kila tovuti unayotembelea.

2. DATA TUNAYOKUSANYA KUKUHUSU

2.1 Data binafsi au taarifa binafsi, inamaanisha taarifa kuhusu mtu binafsi ambapo mtu huyo anaweza kutambulika. Haijumuishi data ambapo utambulisho umeondolewa (data isiyombainisha mtu).

2.2 Tunaweza kukusanya, kutumia, kuhifadhi na kuhamisha aina tofauti za data binafsi kukuhusu ambazo tumepanga pamoja kama ifuatavyo:

โ€ข Data ya Utambulisho inajumuisha jina la kwanza, jina la kati, jina la mwisho, jina la mtumiaji au vibainishi kama hivyo, hali ya ndoa, cheo, tarehe ya kuzaliwa na jinsia.

โ€ข Data ya Mawasiliano inajumuisha anwani, anwani ya barua pepe na nambari za simu.

โ€ข Data ya Kifedha inajumuisha akaunti ya benki na maelezo ya kadi za malipo.

โ€ข Data ya Miamala inajumuisha maelezo ya malipo yaliyofanywa kwako.

โ€ข Data ya Utafiti inajumuisha majibu unayotoa kwenye tafiti tunazokualika ushiriki.

โ€ข Data ya Mawasiliano inajumuisha mawasiliano yako nasi na maoni yoyote unayotoa kuhusu huduma zetu.

2.3 Pia tunakusanya, kutumia na kushiriki Data ya Jumla kama vile data ya kitakwimu au ya kidemografia kwa malengo yoyote. Data ya Jumla inaweza patikana kutoka kwenye data yako binafsi lakini haitambuliki kama data binafsi kisheria na data hii haikutambulishi moja kwa moja au vinginevyo. Kwa mfano, tunaweza weka jumla ya Data yako ya Utafiti kutekeleza utafiti wa data na utafiti wa kitakwimu. Lakini, tukijumuisha au kuunganisha Data ya Jumla pamoja na data yako ya binafsi ili iweze kukutambulisha moja kwa moja au vinginevyo, tunachukulia data ya kujumuishwa kama data binafsi ambayo itatumika kulingana na ilani hii ya faragha.

2.4 Tutakusanya tu Kategoria Maalumu ya Data Binafsi kukuhusu (hii inajumuisha maelezo kuhusu mbari au kabila lako, imani za kidini au za kifilosofia, maisha ya ngono, mwelekeo wa kijinsia, maoni ya kisiasa, ushiriki wa muungano wa biashara, taarifa kuhusu afya yako na jenetiki na data ya kibiometriki) au taarifa kuhusu hatia ya uhalifu na makosa kwa idhini yako moja kwa moja, na kama tu ina uhusiano muhimu na utafiti, kama sehemu ya Data ya Utafiti.

2.5 Endapo hupendelei kutoa data binafsi wakati unapoombwa, unaweza kukosa kushiriki katika utafiti huu na kupokea motisha au manufaa mengine kwa kushiriki katika utafiti.

3. DATA YAKO BINAFSI INAKUSANYWA KWA JINSI GANI

3.1 Tunatumia njia tofatui kukusanya data kukuhusu na kutoka kwako ikijumuisha kupitia:

โ€ข Mwingiliano wa moja kwa moja. Unaweza kutupatia utambulisho wako, Mawasiliano, Data ya Kifedha na ya Utafiti kwa kujaza fomu au kwa kuwasiliana nasi kupitia posta, simu, barua pepe au vinginevyo. Hii inajumuisha data binafsi unayotoa wakati unaposhiriki katika tafiti zetu au ukitupatia maoni fulani.

โ€ข Teknolojia au mwingiliano wa kiotomatiki. Wakati unapoingiliana na tovuti yetu, tunaweza kukusanya kiotomatiki Data ya Kiufundi na Data ya Matumizi kuhusu kifaa chako, vitendo na ruwaza za kuvinjari. Tunakusanya data hii binafsi kwa kutumia vidakuzi, kumbukumbu za seva na teknolojia zingine sawia. Pia tunaweza kpokea Data ya Kiufundi kukuhusu kama utatembelea tovuti zingine zinazotumia vidakuzi vyetu. Unawezakupangilia kivinjari chako kikatae vidakuzi vyote au kadhaa vyakuvinjari, au kukuarifu wakati tovuti zinaweka au kufikia vidakuzi. Endapo unalemaza au kukataa vidakuzi, tafadhali tambua kwamba sehemu zingine za tovuti hii hutaweza kuzifikia au hazitafanya kazi vizuri. Tafadhali angalia Sera yetu ya Vidakuzi kwa maelezo zaidi.

โ€ข Wahusika Wengine au vyanzo vingine vinavyopatikana kwa umma. Tunaweza kupokea data binafsi kukuhusu kutoka kwa wahusika wengine tofauti na vyanzo vya umma kama ilivyoelezwa hapo chini:

โ€“ Utambulisho na Data ya Mawasiliano kutoka kwa madalali wa data au wajumuishaji wa Umoja wa Ulaya.

โ€“ Utambulisho na Data ya Mawasiliano kutoka kwenye vyanzo vinavyopatikana kwa umma kama vile Mamlaka ya Kusajili Kampuni na Rejista ya Wapigaji Kura ndani ya Umoja wa Ulaya.

4. JINSI TUNAVYOTUMIA DATA YAKO BINAFSI

4.1 Tumeweka hapa chini, katika muundo wa jedwali, maelezo ya njia zote tunazopanga kutumia data yako binafsi, na ni kwa misingi gani ya kisheria tunategemea kufanya hivyo. Pia tumebainisha ni yapi maslahi yetu halali pale inapowezekana.

4.2 Tambua kwamba tunaweza kuchakata data yako binafsi kwa zaidi ya msingi mmoja wa kisheria kulingana na matumizi maalum ambayo tunatumia data yako. Tafadhali wasiliana nasi kama unahitaji maelezo kuhusu msingi maalum wa kisheria tunaotumia kuchakata data yako binafsi ambapo zaidi ya msingi mmoja imepangwa katika jedwali hapa chini.

4.3 Bofya hapa kuelewa zaidi kuhusu aina tofauti za misingi ya kisheria tunazoweza kutumia kuchakata data yako binafsi.

4.4 Mabadiliko ya Kusudi

Tutatumia data binafsi kwa malengo ambayo tumekusanyia, isipokuwa tutaona kwamba tunaihitaji kwa matumizi mengine na sababu hizo zinaambatana na lengo la asili. Kama ungependa kupata maelezo ya jinsi mchakato wa lengo jipya unaambatana na lengo asili, tafadhali wasiliana nasi.

Kama tunahitaji data yako binafsi kwa malengo yasiyohusiana, tutakuarifu na kueleza msingi wa kisheria ambao unatukubalia kufanya hivyo.

Tafadhali elewa kwamba tunaweza kuchakata data yako binafsi bila idhini au wewe kuelewa, kwa kuzingatia sheria zilizo hapo juu, wakati hili limehitajika au kukubaliwa kisheria.

5. UFICHUZI WA DATA YAKO BINAFSI

5.1 Inaweza kutubidi kushiriki data yako binafsi pamoja na washirika waliowekwaa hapo chini kwa malengo yaliyopangwa katika jedwali katika aya ya 4 hapo juu.

โ€ข Tunaweza pia kufichua taarifa kwa Yonder Consulting Limited Group yenye makao Uingereza inayofanya kazi kama mdhibiti mwenza endapo utafiti unatekelezwa kwa niaba ya kampuni ya Yonder Consulting Limited Group mbali na Yonder Data Solutions.

โ€ข Watoa huduma wanaofanya kazi kama wachakataji wenye makao Uingereza ambao wanatoa huduma za Teknolojia na usimamizi wa mfumo.

โ€ข Washauri wa kitaalamu wanaofanya kazi kama wachakataji au wadhibiti ikijumuisha wanasheria, benki, wakaguzi na watoa huduma za benki wenye makoa Uingereza wanaotoa huduma za ushauri, kibenki, sheria, bima na uhasibu.

โ€ข Mapato ya HM & Forodha, wadhibiti na mamlaka mengine wanaofanya kazi kama wachakataji au wadhibiti wenye makao Uingereza wanaohitaji ripoti ya shughuli za mchakato katika hali fulani.

โ€ข Kampuni za kidemografia kijiografia kama vile Experian zinazofanya kazi kama wachakataji wanaoishi Uingereza wanaotupatia uchambuzi na maoni ya ziada kwenye tafiti zetu.

โ€ข Wahusika wengine ambao tunaweza kuwauzia, kuwahamishia au kuunganisha sehemu za biashara au rasilimali zetu. Vinginevyo, tunaweza tafuta kupata biashara zingine au kuungana nazo. Kama mabadiliko yatafanyika kwenye biashara yetu, basi wamiliki wapya wanaweza kutumia data yako binafsi kwa njia sawia iliyowekwa katika ilani hii ya faragha.

5.2 Isipokuwa tumekuarifu mwanzoni wa utafiti huu au tumepokea idhini yako kama sehemu ya utafiti, hatufichui Data ya Utafiti ambayo ni binafsi kwa wateja wetu. Data ya Utafiti haibainishwi na mtu na kushirikiwa na wateja wetu na wahusika wengine kwa njia ya kijumla ambayo haikutambulishi. Kwa mfano: โ€œWatu 8 kati ya 10 huko Uingereza wanafurahia kazi zao kwa sasaโ€.

5.3 Tunahitaji wahusika wengine wote kuheshimu usalama wa data yako binafsi na kuichakata kulingana na sheria. Hatukubalii watoa huduma wetu wengine watumie data yako binafsi kwa malengo yao wenyewe na tunawaruhusu wachakate taarifa yako binafsi pekee kwa malengo maalum na kulingana na maelekezo yetu.

6. UHAMISHAJIWA KIMATAIFA

6.1 Wakati wowote tunaposafirisha data yako binafsi nje ya EEA, tunahakikisha kiwango sawia cha ulinzi kimetolewa kwake kwa kuhakikisha angalau moja wapo ya ulinzi huu ufuatao umetekelezwa:

โ€ข Tutasafirisha data yako binafsi pekee kwa nchi ambazo zimechukuliwa kutoa kiwango cha kutosha cha ulinzi wa data za binafsi kupitia Tume ya Uingereza. Kwa maelezo zaidi, angalia Tume ya Uingereza: Ukamilifu wa ulinzi wa data binafsi kwa nchi zisizo za Uingereza.

โ€ข Wakati tunapotumia watoa huduma fulani, tunaweza kutumia mikataba maalum iliyoidhinishwa na Tume ya Uingereza ambayo inatoa kwa data binafsi ulinzi sawia kama huko Uingereza. Kwa maelezo zaidi, angalia Tume ya Uingereza: Mifano ya mikataba ya uhamishaji wa data binafsi kwa nchi zingine.

โ€ข Tunapotumia watoa huduma wa Marekani, tunaweza kuhamisha data kwenda kwao endapo hao ni sehemu ya Ulinzi wa Faragha ambayo inawahitaji kutoa ulinzi sawia unaotumika kati ya Uingereza na Marekani. Kwa maelezo zaidi, angalia Tume ya Uingereza: Uingereza-Marekani Ulinzi wa Faragha.

6.2 Tafadhali wasiliana nasi kama unataka taarifa zaidi kuhusu njia maalum tunayotumia wakati wa kuhamisha data yako binafsi nje ya EEA.

7. USALAMA WA DATA

7.1 Tumeweka mikakati mwafaka ya usalama kuzuia data yako binafsi kupotea kwa bahati mbaya, kutumika au kufikiwa kwa njia isiyoidhinishwa, kubadilishwa au kufichuliwa. Aidha, tunapunguza ufikiaji kwa data yako binafsi kwa wafanyakazi, mawakala, wakandarasi na wahusika wengine ambao wanamahitaji ya kibiashara ya kujua. Watachakata data yako binafsi kwa maelekezo yetu pekeena wanawajibika kwa faragha.

7.2 Tumeweka utaratibu wa kushughulika ukiukaji wowote unaoshukiwa wa data binafsi na tutakuarifu wewe na mdhibiti yeyote husika kuhusu ukiukaji ambao tunahitajika kisheria kufanya hivyo.

8. UHIFADHI WA DATA

8.1 Utatumia Data Binafsi yangu kwa muda gani?

Tutahifadhi data yako binafsi kwa muda mrefu kadiri inavyowezekana ili kutimiza malengo ya kuikusanya, ikiwemo malengo ya kutimiza mahitaji yoyote ya kisheria, uhasibu au kuripoti.

Kutathmini muda mwafaka kwa kuhifadhi data binafsi, tunazingatia kiwango, hali na umuhimu wa data binafsi, uwezekano wa hatari kwa matumizi yasiyoidhinishwa au ufichuzi wa data yako binafsi, malengo ya kuchakata data yako binafsi na kama tunaweza kutimiza malengo hayo kupitia njia zingine, na mahitaji husika ya kisheria.

Kwa mujibu wa sheria, tunahitaji kuhifadhi taarifa za msingi za washirika wetu wa jopo (ikijumuisha Mawasiliano, Utambulisho, Data ya Kifedha na ya Miamala) kwa miaka sita baada ya wao kusita kuwa washiriki kwa makusudi ya kodi.

Kwa hali fulani unaweza kutomba tufute data: angalia ombi la kufuta hapo chini kwa taarifa zaidi.

Tunaweza kufanya data yako binafsi isikubainishe (ili isiweze kuhusishwa na wewe tena) kwa malengo ya utafiti au takwimu ambapo tunaweza kutumia taarifa hii kwa kudumu bila maelezo ya ziada tena kwako.

9. HAKI ZAKO ZA KISHERIA

9.1 Chini ya hali fulani, una haki chini ya sheria za ulinzi wa data inayohusiana na data yako binafsi.

โ€ข Kuomba ufikiaji kwa data yako binafsi.

โ€ข Kuomba urekebishaji wa data yako ybinafsi.

โ€ข Kuomba kufuta data yako binafsi.

โ€ข Kukataa kuchakata data yako binafsi.

โ€ข Kuomba uzuizi wa kuchakata data yako binafsi.

โ€ข Kuomba kuhamisha data yako binafsi.

โ€ข Haki ya kuondoa idhini.

9.2 Kama unapendelea kutimiza haki zozote zilizo tajwa hapo juu, tafadhali wasiliana nasi.

9.3 Kawaida Hakuna Ada Inayohitajika

Hutahitajika kulipia ada kufikia data yako binafsi (au kutimiza haki zozote zingine). Lakini, tunaweza kutoza ada inayofaa kama ombi lako hali msingi waziwazi, la kurudiwa au limepita kiasi. Vinginevyo, tunaweza kukataa kutimiza ombi lako katika hali hizi.

9.4 Kile tunachoweza kuhitaji kutoka kwako

Tunaweza kuhitaji kuomba taarifa maalum kutoka kwako kutusaidia kuthibitisha utambulisho wako na kuhakikisha haki yako ya kufikia data yako ybinafsi (au kutekeleza haki zako zozote). Hii ni mbinu ya usalama kuhakikisha data yako binafsi haifichuliwi kwa mtu yeyote ambaye hana haki ya kuipokea. Pia tunaweza kukuwasilia kukuuliza taarifa zaidi kuhusiana na ombi lako kuharakisha majibu yetu.

9.5 Kikomo cha Muda Kutoa Majibu

Tunajaribu kujibu maombi yote halali ndani ya mwezi mmoja. Mara kwa mara inaweza kuchukua zaidi ya mwezi kama ombi lako lina changamoto maalumu au una maombi kadhaa. Katika kesi hii, tutakuarifu na kukujulisha.

10. FAHARASA

10.1 โ€ข Idhini ya Msingi wa Kisheria inamaanisha kuchakata data yako ambapo tumepokea ruhusa yako iliyotolewa kw hiari, mahususi, na bila utata wowote. Unaweza kuondoa idhini yako wakati wowote halafu tutaacha kuchakata taarifa yako kwa lengo hilo.

โ€ข Masilahi Halali inamaanisha masilahi ya biashara yetu kwa kuendesha na kudhibiti biashara yetu kutuwezesha kukupatia bidhaa/huduma bora zaidi na uzoefu salama zaidi. Tunahakikisha tunazingatia na kuweka uwiano wa athari yoyote inayowezekana kwako (hasi na chanya) na haki zako kabla ya kuchakata data yako binafsi kwa masilahi yetu halali. Hatutumii data yako binafsi kwa shughuli ambapo masilahi yako yamefutwa na athari kwako (isipokuwa kama umetupatia idhini au vinginevyo unahitajika au kuruhusiwa kisheria). Unaweza kupokea taarifa zaidi kuhusu jinsi tunatathmini masilahi yetu halali dhidi ya uwezekano wa athari yeyote kwako kuhusiana na shughuli maalumu kwa kuwasiliana nasi.

โ€ข Utendaji wa Mkataba inamaanisha kuchakata data yako wakati inahitajika kwa ajili ya utekelezaji wa mkataba ambapo wewe ni mshirika au kuchukua hatua kwa ombi lako kabla ya kuingia katika mikataba hiyo.

โ€ข Kuzingatia wajibu wa kisheria sheria au kiudhibiti inamaanisha kuchakata data yako binafsi wakati inahitajika kwa ajili ya ufuatiliaji wa sheria au kufuata maagizo ambayo tunapaswa kuzingatia.

10.2 Haki Zako za Kisheria

Uko na haki ya:

โ€ข Kuomba kufikia data yako binafsi (kawaida inajulikana kama โ€œombi la ufikiaji la mhusika wa dataโ€). Hii inakuwezesha kupokea nakala ya data binafsi tunayohifadhi kukuhusu na kuagalia kwamba tunaichakata kisheria.

โ€ข Kuomba urekebishaji wa data binafsi ambayo tumehifadhi kukuhusu. Hii inakuwezesha kuwa na data yoyote isiyo kamili au isiyo sahihi ambayo tumeihifadhi kukuhusu kurekebishwa, ingawa tunaweza kuhitaji kuhakiki usahihi wa data mpya unayotupatia.

โ€ข Kuomba kufuta data yako binafsi. Hii inakuwezesha kutuomba kufuta au kuondoa data binafsi ambapo hakuna sababu nzuri kwetu kuendelea kuichakata. Pia una haki ya kutuomba kufuta au kuondoa data yako binafsi wakati umefanikiwa kutimiza haki yako kukataa uchakataji (angalia hapa chini), ambapo kama tumechakata taarifa yako bila kufuata sheria au ambapo inahitajika kufuta data yako binafsi ili kuzingatia sheria ya eneo husika. Tambua, hata hivyo, kila mara tutaweza kutekeleza ombi lako la ufutaji kwa sababu maalum za kisheria ambazo utaarifiwa, kama zipo, wakati wa ombi lako.

โ€ข Kupinga uchakataji wa data yako binafsi wakati tunategemea masilahi yako halali (au yale ya mhusika mwingine) na kuna jambo fulani kuhusu hali yako maalum ambayo inakufanya utake kupinga uchakataji kwa msingi huu kwa vile unahisi unaathiri uhuru na haki zako za msingi. Pia una haki ya kupinga ambapo tunachakata data yako binafsi kwa malengo ya soko ya moja kwa moja au endapo tunachakata data yako binafsi kwa malengo ya utafiti wa takwimu, isipokuwa kama uchakataji huo ni muhimu kwa masilahi ya umma. Katika kesi fulani, tunaweza kuonyesha kwamba tukoa na misingi halali yakushawishi kuchakata taarifa yako ambayo inapingana na haki na uhuru wako.

โ€ข Kuomba kuzuia uchakataji wa data yako binafsi. Hii inakuwezesha kutuomba tusitishe mchakato wa data yako binasi katika hali zifuatazo: (a) kama unataka tuhibitishe usahihi wa data; (b) wakati matumizi yetu ya data ni kinyuma cha sheria lakini hutaki sisi tuifute; (c) wakati unataka sisi tuhifadhi data hata kama hatuihitaji tena kwa vile unaihitaji kuthibitisha, kutekeleza au kutetea madai ya kisheria; au (d) au umepinga matumizi yetu ya data yako lakini tunahitaji kuthibitisha kama tuna misingi halali kuitumia.

โ€ข Kuomba uhamishaji wa data yako binafsi kuja kwako au kwa mhusika mwingine. Tutakupatia au mhusika mwingine uliyechagua, data yako binafsi imepagiliwa, inatumika mara nyingi, kwa muundo unaosomeka kwa mashine. Tambua haki hii inatumika pekee kwa taarifa ya kiotomatiki ambayo awalli ulitoa idhini kwetu kutumia au pale tunapotumia taarifa kutekeleza mkataba nawe.

โ€ข Kuondoa idhini wakati wowote tunapotegemea idhini ya kuchakata data yako binafsi. Lakini, hii itaathiri uhalali wa uchakataji wowote unaotekelezwa kabla ya kuondoa idhini yako. Kama utaondoa idhini yako, hatutaweza kutoa bidhaa au huduma fulani kwako. Tutakushauri kama hali ndiyo hiyo wakati unapoondoa idhini yako.